Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Ufaransa, Alexander Grushko, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema katika mkutano na Pierre Lévy, balozi wa Ufaransa huko Moscow, kuhusu upelekaji wa silaha nchini Ukraine, kwamba utawala wa Kiev hutumia silaha hizo kushambulia taasisi za miji na miundombinu.Kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Grushko na Levy pia walijadili hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa makubaliano ya usafirishaji nafaka na matatizo yanayohusiana na jinsi ya kutoa hakikisho la usalama wa chakula.Katika mkutano na balozi wa Ufaransa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alisisitiza haja ya kuondolewa vikwazo haramu walivyowekewa wazalishaji wa nafaka na mbolea za kemikali nchini Russia, na vilevile kuondolewa vizuizi vya kusambaza bidhaa kwenye masoko ya nchi zinazoendelea ili kuzuia matokeo hasi na mabaya ya kibinadamu.Putin
Hivi karibuni, Rais Vladmir Putin wa Russia alitangaza kwamba nafaka nyingi zinazosafirishwa kutoka bandari za Ukraine zinapelekwa Ulaya badala ya kupelekwa katika nchi maskini na zenye uhitaji, na akautuhumu Umoja wa Ulaya kwamba umezuia tani 300,000 za mbolea za kemikali za Russia kuingizwa katika nchi nyingi masikini duniani.
Vita kati ya Russia na Ukraine vilianza Februari 24.Nchi za Ulaya na Marekani zimechochea na kukoleza moto wa vita na mapigano nchini humo kwa kuzidisha mashinikizo ya vikwazo dhidi ya Russia na kuipatia Kiev kila aina ya silaha nyepesi na nzito...342/